WS14 – WorldSports14

AJAX WAYEYUSHA KOMBE LAO NA KUWAPA MASHABIKI

Klabu ya Ajax imeamua kuliyeyusha kombe lao ubingwa wa ligi kuu ya Uholanzi msimu huu na kutengeneza nyota za ubingwa “Champion Star” ambazo watazigawa kwa shabiki wao wote 42,390 wanaoshikilia tiketi za msimu mzima.

Katika kusheherekea kuongeza rekodi yao ya kuchukua mara nyingi (35) ubingwa wa ligi hiyo, Ajax wameamua kutengeneza nyota hizo za kumbukumbu ambapo moja ina uzito wa gramu 3.45.

Ajax wamesema wamefanya hivyo ili kuonesha kutambua mchango wa washabiki licha ya kushindwa kuhudhuria uwanjani kutokana na uwezo wa virusi vya Corona

Pia timu hiyo imethibitisha shirikisho la soka la Uholanzi limewapa mfano wa kombe hilo (Replica) ambalo ndilo wataliweka katika kabati la vikombe la klabu.

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More