WS14 – WorldSports14
  • Home
  • Football
  • ODOI AELEZA UGONJWA WA CORONA KUUMWA HADI KUPONA

ODOI AELEZA UGONJWA WA CORONA KUUMWA HADI KUPONA

Winga wa klabu ya Chelsea Callum Hudson-Odoi amezungumza kuhusiana na hali yake na mtazamo wake kuhusu kusimama kwa Ligi Kuu England wakati huu akiwa ametoka karantini baada ya kupona corona.

Odoi ambaye alikuwa mchezaji wa kwanza kugundulika kuwa na virusi hivyo, ameeleza alivyokuwa anajiakia na kusema kuwa anafikiri ni vyema Ligi (EPL) ikarejea wakati ambao ni salama zaidi.

”Najisia vizuri sasa nilikuwa na virusi ambavyo vimeondoka sasa, najisikia vizuri, najisikia fiti nahisi nimerudi kuwa kama nilivyokuwa kila kitu kipo sawa”

”Nataka kuona soka linarejea mapema iwezekanavyo ningependa kuona mchezo wa mpira wa miguu unaendelea kuchezwa leo kama ingewezekana lakini hii kitu (virusi) inakuwa na kuendelea tunachokitaka ni kutaka kuona watu wanaendelea vizuri”

This website uses cookies to improve your experience. We'll assume you're ok with this, but you can opt-out if you wish. Accept Read More